TIST Tanzania Newsletter - March 2024

Newsletter PDF (Large File!)
Newsletter Content
TIST HABARI MOTOMOTO MARCH 2024
www.tist.org. Email: info@tist.org Tel. +255784-537720

(i)Verification and Validation Postponement

TIST Program Tanzania had announced the validation and verification exercise that was supposed to start in April 2024. We have been informed by the Verifiers that the exercise has been postponed so it will not happen in April. The Verifiers are scheduling another time in the next few weeks and we will let you know on the dates once it is scheduled. Let us continue working hard on our farms as we wait for our Verifiers visitation.

In this newsletter, we are going to have a notification, an article and a story:

(i) Verification and Validation Postponement for the TIST Program Tanzania.
(ii) The process to follow for new farmers who wants to join TIST and things they need to do before joining TIST.
(iii) A story from Rafael Chinolo about how he earned income from selling seedlings, fruits, fish and honey that helped him build a house purchased a motorcycle and a Television.

(i)The process to follow for new farmers who wants to join TIST and things they need to do before joining TIST

Interested Farmers who want to join TIST will contact any TIST Servant. They will need to form a Small Group of 6-12 close neighbors. 

A TIST Servant will train you about what is TIST and Small Group Formation Your new Small Group will need to start doing weekly meetings (at Small Group Level) and also attending Monthly Cluster Meetings.

Training for a New Small Group
Your Small Group will be guided through the Application Process and taught about Small Groups Best Practices (weekly meetings, Rotational & Servant leadership, Kujengana, Action planning, Raised Nursery Management, bee hives, hygiene, etc.

Each member of your Small Group should beattending a Cluster meeting every month. Your Small Group will be issued with Application Process document.

Things that each of your Small Group members need to learn and understand during Application Process.

1. Each member should learn and understand Tree species and their importance (You will also be trained on Trees that do not qualify for carbon).

2. Each member should learn and understand how to establish Tree Nurseries.

3. Each member of your Small Group should be attending Weekly Small Group meetings using TIST Best Practices.

4. Your Small Group should start practicing Rotational and Servant Leadership and Kujengana.
5. Each member should learn and understand how to practice Conservation Farming.
6. Each member should learn and understand Greenhouse Gas (GhG) Contract.
7. Each member should learn and understand Small Group Eligibility Requirements.
Your Cluster Servant will use pendragon form to register your Small Group as Applicant Group.

Cluster Trainings and meetings
Your Small Group members should attend Cluster Trainings every month
At the Cluster meeting, Cluster Servants and Cluster Leaders should work together to provide TIST members with high Quality Trainings, provide them
with latest TIST News and Information, Answer their Questions, Concern and or Grievances. They should also communicate with TIST Leadership on any
requests Cluster members may have. 

Additionally, Cluster Servants should update in the TIST Mobile Website, the Cluster meeting dates, dates of election and Cluster Leaders information. 

Each Cluster should rotate Leadership after every four months. Cluster leader rotates out, Co-Leader becomes Leader and new Accountability person is elected. If Co-leader is a Male, Accountability should be a Female and vice-versa .

Cluster Servants and Leaders should welcome new members at the Cluster meeting.

Cluster Servant should each month make arrangements with Small Groups members that will have their trees quantified till the next Cluster meeting.


Cluster Servant should at every Cluster Meeting notify each Small Group their current status Profit share eligibility, number of Groves and trees Quantified etc.

Baseline for New Small Group

Your Small Group members should identify areas they want to plant trees now and in future.

Your Small Group members should be presentwhen a Cluster Servants come to take
Baseline (To answer Questions related to ownership, history of the land etc).

Baseline yields to getting the Grove into a PDD(Project Design Document).
This is the first step in participating in carbon credit business.

Baseline involves answering questions about the Grove area a farmer has identified for planting
- Ownership (Please show a Title Deed, Permission from land owner, Customary, Lease)
(The right to plant the trees on the land is required for the Grove to Qualify)
- Forest. Whether a Grove is already a Forest (If Yes, the Grove cannot Qualify)
- Deforested (If the grove was a forest, and was cut down in the10 years before joining TIST). If yes, Grove cannot qualify
- Displacement. If a farmer is stopping other activities so as to plant trees for carbon, this Grove cannot qualify
- Topography
- Baseline Trees and baselines Stumps (Baseline trees and trees that sprout from Baseline stumps are not quantified as TIST Trees)
- Tracks – Primary track 1 and track 2. Your Cluster Servant will only take track when satisfied your Grove meets all Baseline Requirements Your Cluster Servant will also take GPS Readings at the center of the Grove.
If the Grove doesn’t qualify, Cluster Servant should inform you the reasons.

Registration of your Small Group

Your Small Group will be formally registered in TIST after all members have passed Application Process and all are voluntarily joining TIST.

After your Group has been successfully baselined, pass Application process and meets all Small Group Eligibility requirements, you shall;

a) Re-read, understand, sign the Greenhouse Gas (GhG) Contract
b) Your Cluster Servant will have the contract uploaded in the TIST Website
c) Your Small Group should retain and keep safe, the original copy of GhG Contract
d) Your Cluster Servant will register your Group using the Pendragon Form

(ii) A story from Rafael Chinolo about how he earned income from selling
seedlings, fruits, fish and honey that helped him build a house, bought a
motorcycle and a Television.

As a TIST Farmer, Rafael Chinolo has chosen to plant trees, growing seedlings for sale as well as keeping bees and fish.

His Small Group is Mazingira with TIST number 2000TZ52 found in Chamkoroma village, Kongwa district. He has planted a total of 870 trees in his farm.

Rafael has planted different tree species which include Jacaranda, Neem, Teak, Scented cassia, African mahogany, and other varieties such as Mango, Avocado, Java plum, orange, lemon, guava, cashew trees, etc. that provide him with
different fruits, nuts, fresh air, medicines, firewood, and place for keeping beehives. Apart from having trees and seedlings, he also keeps beehives in his grove that provide him with honey for selling and for home consumption; keeps fish in a pond which he dug just few meters from his house.

The money he earns from selling seedlings, fruits, fish, and honey has helped Rafael to build a house, purchased a motorcycle and a television. Also he is able to purchase food that he is not able to grow and produce on his farm.

Over the past 23 years as a TIST Farmer, Rafael has been a trainer in his community. He provides trainings on environmental education, particularly tree planting, Conservation Farming, and improved cook stoves (majiko banifu) that
can help families, communities, and the environment. From doing all these things Rafael has been awarded with certificates of recognition and appreciations from different organizations such as TIST, District Commissioner’s Office, Prime Minister’s Office, INADES Formation, SNV, etc.

Other farmers and the community around him talk about Rafael that he has become a role model and they use him for instructions, seminars and advice. He is also used to provide education inside and outside his district.

Rafael actively encourages other farmers to keep planting more trees for our own benefit and the environment.

What do we create?
1) We create team work – by doing things this way; we end up working as a team.
2) We create capacity- we create organization, strength, and a system that is strong.
3) We create enjoyment – we see results, we accomplish big things that we enjoy.
4) We create Big Results - Big results in planting trees, in Conservation Farming and from other projects and business that we do.
5) We create Low Budget/Cost, yet we achieve big results.

TIST VALUES
1) We are Honest.
2) We are Accurate.
3) We are Transparent
4) We are Servants to each other.
5) We are Mutually Accountable to Each Other.
6) Low Budget, Big Results.

What do we do?
1) We plant different species of trees for long – term.
2) We find ways to improve our health.
3) We practice Conservation Farming.
4) We do other projects and businesses (sustainable agriculture, nurseries, citrus
growing, dairy goats and farming, chickens, bee keeping, fishponds and fish keeping, silkworm farming etc.)
5) We sell carbon credits.

INTRODUCTION OF CLUSTER SERVANT

We are introducing Cluster Servant BARAKA MAGUBI from Tubugwe village Kongwa district. He joined TIST in the year 2022. He is a farmer from Hekima Group TIST number 2004TZ731.

Baraka serves four (4) Clusters: Tubugwe, Chamkoroma, Mseta and Tambi Clusters. Experienced in farming, quantification (tree counting), recruitment of new Small Groups and data entry into Pendragon. He is also managing farmers and instructing them on Conservation Farming provides TIST seminars to the Small Groups across the whole TIST Program in Tanzania.

If you have any questions, or you need help on how to join the TIST Program, you may contact him through; 0629513140 or 0628651802.

TIST HABARI MOTOMOTO MACHI 2024
www.tist.org. Email: info@tist.org Tel. +255784-537720

(i) Kuahirishwa kwa zoezi la Uhakiki na Uthibitishaji

Mpango wa TIST Tanzania ulikuwa umetangaza zoezi la uhakiki na uthibitishaji ambalo lilipaswa kuanza mwezi Aprili 2024. Tumefahamishwa na Wahakiki kuwa zoezi hilo limeahirishwa hivyo halitafanyika mwezi wa Aprili kama ilivyokuwa imepangwa. Wathibitishaji wanapanga kufanya zoezi hili wakati mwingine katika wiki chache zijazo. Hivyo tutawajulisha tarehe pindi ratiba itakapotoka. 

Kipindi hiki tuendelee kufanya kazi kwa bidii kwenye mashamba yetu tunaposubiri kutembelewa na Wathibitishaji.

Katika jarida hili, tutakuwa na taarifa, makala na hadithi:
(i) Kuahirishwa kwa zoezi la Uhakiki na Uthibitishaji
(ii) Utaratibu wa kufuata kwa wakulima wapya wanaotaka kujiunga na TIST na mambo wanayohitaji kufanya kabla ya kujiunga na TIST
(iii) Hadithi kutoka kwa Rafael Chinolo kuhusu jinsi alivyopata mapato kutokana na kuuza miche, matunda, samaki na asali, mapato hayo yalimsaidia kujenga nyumba, kununua pikipiki na Televisheni.

(i) Utaratibu wa kufuata kwa Wakulima wapya wanaotaka kujiunga na TIST na mambo wanayohitaji kufanya kabla ya kujiunga na TIST

Mkulima anayetaka kujiunga na TIST atawasiliana na Mtumishi yeyote wa TIST. Mkulima atahitajika kuunda Kikundi Kidogo kuanzia watu 6-12 walio majirani.

Mtumishi wa TIST atakufundisha kuhusu TIST na Uundaji wa Kikundi Kidogo. Kikundi chako kipya kitahitajika kuanza kufanya mikutano ya kila wiki (katika Ngazi ya Vikundi Vidogo) na pia kuhudhuria Mikutano ya Klasta Kila Mwezi.

Mafunzo kwa Kikundi Kidogo Kipya

Kikundi chako Kidogo kitaongozwa kupitia utaratibu wa Maombi na kufundishwa kuhusu Mbinu Bora za Vikundi Vidogo (mikutano ya kila wiki, Uongozi wa Mzunguko na Kujengana, Mpango kazi, Usimamizi wa vitalu vilivyoanzishwa n.k.

Kila mwanachama wa Kikundi chako Kidogo anapaswa kuhudhuria mkutano wa Klasta kila mwezi. Kikundi chako Kidogo kitapewa fomu ya utaratibu wa Maombi.

Mambo ambayo kila mjumbe wa Kikundi chako Kidogo anahitaji kujifunza
na kuelewa wakati wa Mchakato wa Maombi.

1. Kila mwanachama anapaswa kujifunza na kuelewa aina za Miti na umuhimu wake (Utafunzwa pia kuhusu Miti ambayo haistahiki kaboni).

2. Kila mwanachama ajifunze na kuelewa jinsi ya kuanzisha Vitalu vya Miti

3. Kila mwanachama wa Kikundi chako Kidogo anapaswa kuhudhuria mikutano ya Kila Wiki ya Kikundi Kidogo kwa kutumia Mbinu Bora za TIST.

4. Kikundi chako Kidogo kianze kufanya Uongozi wa Mzunguko, Kutumikiana na Kujengana

5. Kila mwanachama ajifunze na kuelewa jinsi ya kufanya Kilimo Hai

6. Kila mwanachama anapaswa kujifunza na kuelewa Mkataba wa GhG

7. Kila mwanachama anapaswa kujifunza na kuelewa Mahitaji ya Kustahiki kwa Kikundi Kidogo

 Mtumishi wako wa Klasta atatumia fomu ya pendragon kusajili Kikundi chako Kidogo kama Kikundi kilichotuma maombi.

Mafunzo ya Klasta na mikutano

Wanakikundi chako Kidogo wanapaswa kuhudhuria Mafunzo ya Klasta kila mwezi

Katika mkutano wa Kikundi, Watumishi wa Klastana Viongozi wa Klasta wanapaswa kufanya kazipamoja ili kuwapa wanachama wa TIST Mafunzo ya Ubora wa hali ya juu, kuwapa Habari na Taarifa za TIST za hivi punde, Kujibu Maswali, Wasiwasi na au Malalamiko yao. Pia wanapaswa kuwasiliana na Uongozi wa TIST juu ya maombi yoyote ambayo wanachama wa Kikundi wanaweza
kuwa nayo.

Pia, Watumishi wa Klasta wanapaswa kuchapisha katika Tovuti ya TIST Mobile, tarehe za mikutano ya Klasta, tarehe za uchaguzi na taarifa za Viongozi
wa Klasta.
Kila Klasta inapaswa kubadilisha Uongozi kila baada ya miezi minne.

Watumishi wa Klasta na Viongozi wanapaswa kuwakaribisha wanachama wapya kwenye mkutano wa Klasta.

Kila mwezi Mtumishi wa Klasta lazima aweke mipango vizuri na Wanavikundi Vidogo ambavyo miti yao itahesabiwa hadi mkutano ujao wa Klasta.

Katika kila Mkutano wa Kikundi Mtumishi wa Klasta anapaswa kuarifu kila Kikundi Kidogo hali yao ya sasa ya kustahiki ugawaji wa Faida, idadi ya Mashamba na miti iliyokadiriwa n.k.

Taarifa za awali za Kikundi Kidogo Kipya

Wanakikundi wanapaswa kutambua maeneo wanayotaka kupanda miti sasa na siku zijazo.

Washiriki wa Kikundi wanapaswa kuwepo wakati Watumishi wa Klasta wanakuja kuchukua taarifa za awali (Kujibu Maswali yanayohusiana na umiliki, historia ya ardhi n.k)

Matokeo ya taarifa za awali za shamba zitasaidia kupata Hati ya Usanifu wa Mradi. Hii ni hatua ya kwanza katika kushiriki katika biashara ya kaboni

Taarifa za awali zinahusisha kujibu maswali kuhusu eneo la shamba ambalo mkulima ametenga kwa ajili ya kupanda miti.

- Umiliki (Tafadhali onyesha Hati miliki, Ruhusa kutoka kwa mmiliki wa ardhi, Kimila, Kukodisha). (Ikiwa hakuna umiliki uliothibitishwa, shamba halitakuwa na vigezo.

- Miti ya awali na Visiki vya awali (Miti ya awali na miti inayochipuka kutoka kwenye visiki vya awali haitatambuliwa kama Miti ya TIST).

- Mzunguko wa shamba – Mzunguko wa 1 na wa 2. Mtumishi wako wa Klasta atachukua taarifa za shamba lako endapo tu limekidhi vigezo vyote wakati wa kuchukua taarifa za awali.

Mtumishi wako wa Klasta pia atachukua namba ya GPS katikati ya shamba.

Ikiwa shamba halistahiki, Mtumishi wa Klasta anapaswa kukujulisha sababu.

Usajili wa Kikundi chako Kidogo

Kikundi Kidogo kitasajiliwa rasmi TIST baada ya wanachama wote kupitia utaratibu wa Maombi na wote wanajiunga na TIST kwa hiari.

Baada ya Kikundi chako kuanzishwa kwa ufanisi, kupitisha mchakato wa Maombi na kukidhi mahitaji yote ya Kustahiki kwa Kikundi Kidogo, utalazimika;

a) Kusoma tena, kuelewa, kutia saini Mkataba wa Gesi ya Greenhouse ( GhG).
b) Mtumishi wako wa Klasta ataweka mkataba katika Tovuti ya TIST
c) Kikundi chako Kidogo kinapaswa kuhifadhi na kuweka salama, nakala halisi ya Mkataba wa GhG
d) Mtumishi wako wa Klasta atasajili Kikundi chako kwa kutumia Fomu ya Pendragon Baada ya kupitia na kumaliza hatua zote hizi kikundi chako kitakuwa kimesajiliwa rasmi na TIST.

(ii) Hadithi kutoka kwa Rafael Chinolo ambaye amepata mapato kutokana na
kuuza miche, matunda, samaki na asali, mapato hayo yalimsaidia kujenga
nyumba, kununua pikipiki na Televisheni.

Kama Mkulima wa TIST, Rafael Chinolo alichagua kupanda miti, kuotesha miche kwa ajili ya kuuza na pia kufuga nyuki na samaki.

Kikundi chake Kidogo ni Mazingira chenye TIST namba 2000TZ52 kinachopatikana katika kijiji cha Chamkoroma, wilayani Kongwa. Amepanda
jumla ya miti 870 katika shamba lake.

Rafael amepanda aina mbalimbali za miti ambayo ni pamoja na Mijakaranda, Miarobaini, Mitiki, Mikasia, Mikangazi, Miashoki, na aina nyinginezo kama vile Miembe, Miparachichi, Mizambarau, Michungwa, Ndimu, Mipera, Mikorosho n.k Miti hii inampatia matunda mbalimbali, hewa safi, madawa, kuni, na mahali pa kuweka mizinga ya nyuki, miti kwa ajili ya kujengea na kutengenezea samani, nk.

Mbali na kuwa na miti na miche, pia ameweka mizinga ya nyuki kwenye shamba lake inayompatia asali kwa ajili ya kuuza na matumizi ya nyumbani. Pia amefuga samaki kwenye bwawa ambalo alichimba mita chache tu kutoka nyumbani kwake.

Pesa anazopata kwa kuuza miche, matunda, samaki na asali zimemsaidia Rafael kujenga nyumba, kununua pikipiki na televisheni. Pia ana uwezo wa kipato cha ziada kinachomsaidia kununua chakula ambacho hawezi kulima na kuzalisha katika shamba lake.

Katika kipindi cha miaka 23 kama Mkulima wa TIST, Rafael amekuwa akitumika maeneo mbalimbali kama mkufunzi. Ni mzoefu wa kutoa mafunzo kuhusu elimu ya mazingira, hasa upandaji miti, Kilimo Hifadhi, na majiko ya kupikia yaliyoboreshwa (majiko banifu) ambayo yanaweza kusaidia familia, jamii na mazingira. Kutokana na kufanya mambo haya yote Rafael ametunukiwa vyeti vya kutambuliwa na kuthaminiwa kutoka mashirika mbalimbali kama vile TIST, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Waziri Mkuu, INADES Formation, SNV, n.k.

Wakulima wengine na jamii inayomzunguka wanamzungumzia Rafael kwamba amekuwa mfano wa kuigwa na wanamtumia kwa maelekezo, semina na ushauri. Pia anatumika kutoa elimu ndani na nje ya wilaya yake.

Rafael anawahimiza wakulima wengine kuendelea kupanda miti zaidi kwa manufaa yetu na mazingira.

Tunaunda nini?

1) Tunaunda kazi ya timu—kwa kufanya mambo kwa kufanya kazi kama timu.
2) Tunajenga Uwezo-tunaunda shirika, nguvu, na mfumo ambao ni imara.
3) Tunafanya mambo yanayotufurahisha-tunaona matokeo, tunatimiza mambo
makubwa ambayo tunafurahia
4) Tunafanya mambo yanayoleta matokeo makubwa-matokeo makubwa ya upandaji miti. matokeo makubwa katika Kilimo Hai na matokeo makubwa kutokana na miradi na biashara zingine tunazofanya.
5) Tunatumia gharama ndogo za Utawala, lakini tunapata

MAADILI YA TIST

1) Sisi ni Waaminifu
2) Sisi Tunatoa Taarifa Sahihi
3) Sisi ni Wawazi
4) Sisi Tunatumikiana
5) Sisi ni Wawajibikaji
6) Bajeti Ndogo, Matokeo Makubwa

Tunafanya Nini?

1) Tunapanda aina mbalimbali za miti itakayodumu kwa muda mrefu.
2) Tunafanya mambo kuboresha afya zetu.
3) Tunafanya Kilimo Hai.
4) Tunafanya miradi na biashara zingine.
5) Tunafanya biashara ya hewa ya kaboni.

UTAMBULISHO WA MTUMISHI WA KLASTA (CLUSTER SERVANT)

Tunamtambulisha Mtumishi wa Klasta BARAKA MAGUBI
kutoka kijiji cha Tubugwe wilaya ya Kongwa. Alijiunga na TIST
mwaka 2022. Yeye ni mkulima kutoka Kikundi cha Hekima chenye
namba ya TIST 2004TZ731.

Baraka anatumikia Klasta nne (4): Tubugwe,Chamkoroma,Mseta na
Tambi. Ana Uzoefu wa, Upimaji (kuhesabu miti) kilimo na
Kuviunganisha Vikundi Vidogo Vidogo vipya kwenye Mpango wa
TIST na kuingiza takwimu kwenye Pendragon. Kadhalika ni mzoefu
wa kusimamia wakulima na kuwaelekeza mbinu bora za kilimo na
kutoa semina za TIST kwa Vikundi Vidogo Vidogo katika Mpango
mzima wa TIST nchini Tanzania.

Ikiwa una maswali yoyote, au unahitaji usaidizi jinsi ya kujiunga na
Mpango wa TIST, unaweza kuwasiliana naye kupitia 0629513140 au
0628651802.